Imani tano zisizo za kweli walizo nazo watu kuhusu uandishi vitabu…

Anaandika mwandishi Mbobevu
Godius Rweyongeza
0755848391
https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

Kuna imani tano kwenye ulimwengu wa uandishi ambazo zimezoeleka miongoni mwa watu ambazo si za kweli, ila zimeshika hatamu kama vile ni za kweli. Siku ya leo nipo hapa kuzieleza hizi imani kwa undani na mwisho wa siku kukupa suluhisho jipya kwa imani ambazo umekuwa nazo tokea mwanzo. Kiufupi ni kuwa nataka nizivunje hizi imani zako na nikupe imani mpya kuhusu uandishi wa vitabu, bila kuongeza la ziada, wacha tuzione…

1. Imani ya kwanza ni imani kuwa ili uandike kitabu unapaswa kuwa msomi. Siyo kweli kuwa ili uandike kitabu unapaswa kuwa msomi mwenye shahada kibao. Kuna wasomi wenye shahada nyingi kama hizo hawajaweza kuandika vitabu japo tulikuwa tunategemea kuwa waweze kuandika vitabu vya kutosha na vizuri.

Siyo jukumu langu kumhukumu mtu wala lakini msomi kama Robert Mugabe aliyekuwa na shahada saba tofauti alipaswa pengine kuwa ameandika vitabu vingi… Ila mpaka anaaga dunia hakuwa ameandika kitabu cchochote, ukweli ni kuwa kwenye kuandika kitabu chako unachohitaji siyo shahada. Unahitaji kuwa na ujumbe wowote ule unaoweza kuufikisha kwa watu…

Na wewe huwezi kukosa ujumbe wa kufikisha kwa watu, yaani kuwa ukose ujuzi wowote, ukose kuwa hata na kitu ambacho umekuwa unakifanya kwa siku nyingi…

Kama ukijisikiliza na kama ukijifiatilia vizuri, utakuwa na mengi. Naam mengi sana ya kuandika…

hata hivyo, ifahamike kuwa kama wewe ni msomi ujue pia wewe unategemewa sana kuandika na una mengi ya kuandika. Hivyo kwa ufupi ni kuwa msomi kwa asiye msomi anaweza kuandika kitabu. Unachohitaji ni maarifa sahihi ya namna ya kuandika kitabu chako. Unajiuliza ni kitu gani uandike?

Unaweza pengine ukawa hujui kitu gani uandike, ila mimi nina uhakika, nikikaa na wewe kwa dakika tano mpaka nusu saa, ninaweza kukupa mawazo lukuki ambayo ni ya kipekee kwako tu, ambayo hakuna mwingine mwenye nayo isipokuwa wewe tu. Upo tayari kunipa nafasi ya kukaa na wewe meza moja kwa dakika tano tu? Basi anza kwa kukaa nami kupitia hiki kitabu hapa, kama baada ya kusoma kitabu hiki utajiona huna kitu chochote cha kuandika. Ninaenda kukurudishia hela yako mara mbili. 100% guranteed!

2. Imani ya pili ni kuwa ili uandike kitabu unapaswa kuwa na umri umeenda….au umezeeka.

Sikumbuki ni mtu gani nilikuwa naongea naye siku za karibuni, ila akawa ananiambia kuwa ili kuandika kitabu chako unapaswa kuwa umestaafu na unakaribia kufa, tena nakwambia alinipa mpaka mifano, hahaha. Kuna kipindi watu walikuwa wanaamini ukiandika wosia unakuwa unakaribia kufa, kwa hiyo kijana kama mimi sipaswi kuandika wosia, ila nadhani hizi imani zimeisha jamani au huko kwenu vipi…..

Kuna watu wengi wanaamini kuwa ili uandike kitabu umri wako unapaswa kuwa umeenda. Uwe umestaafu na umefanya mambo katika ngazi ya kitaifa, kama mheshimiwa Mkapa, Mwinyi, Kikwete, na watu wengine wa aina hiyo….

Huwa wanasema hivi hasa wanapozungumzia kuandika historia ta maisha yako.

Ukweli ni kuwa huhitaji kuwa na miaka yote hiyo ili uandike historia ya maisha yako….
Kuna watu wameandika historia za maisha yao bila gata ya kuwa wanefikisha umri huo…

Unachohitaji siyo umri mwingi, bali nia kuamua kuandika kwani vitu vya kuandikia unavyo vingi. Unachohitaji wewe siyo uwe na historia kama ya Mkapa ili uandike historia yako.

Sikiliza, kama historia za watu wote zingekuwa kama za Mheshimiwa Mkapa au Mwinyi, sasa tunakuwa tunahitaji tuandike nini maana kila kitu si kinakuwa kinafahamika.

Lakini ukweli kuwa wewe huKwemda shule mpaka ilipotokea elimu ya watu wazima ndio unafanya historia ya maisha yako kuvutia watu.

Au ukweli kuwa kuna kipindi nyumbani mlikuwa hampati uji ndiyo utafanya historia yako kuwa pekee…

Huhitaji kuwa umesoma shule ya seminari kama Mkapa, ila ukweli kuwa ulisoma shule ya MTAKUJA na mwalimu alikuwa anakuja darasani amelewa na siku nyingine haingii darasani ndiyo unakupa historia ya kipekee.

Huhitaji kuwa ulipata shahada ya kwanza ukiwa na miaka 17, ila ukweli kuwa ulisoma chuo kikuu ukafeli na kufukuzwa ndiyo utafanya historia yako ya kipekee

Sikiliza, watu wengi wanatumua muda mwingi kutaka kuwa kama watu fulani badala ya kutumia muda mwingi kuwa wao wenyeewe. Kuwa wewe, andika kile ulichonacho na historia yako itakuwa ya tofauti. na huo ndiyo upekee ambao tutaukuta kwenye hisoria ya maisha yako..

3. Ninahitaji muda mwingi ili kuandika kitabu changu
Hii ni imani nyingine ambayo watu wanakuwa nayo. mtu anafikiri kwamba anahitaji muda mwingi ili kuandika kitabu chake na kukikamilisha, ukweli ni kuwa huhitaji kuwa na muda mwingi katika namna hiyo ili uweze kuandika kitabu chako. Ukweli mwingine zaidi ni kuwa hakuna mtu ambaye ana muda kama huo, mimi mwenyewe usije kudhani kuwa nina muda mwingi wa kutosha, mfano naandika andiko hili ukiwa ni usiku saa kumi kasoro dakika 18. Jana nililala saa tano baada ya kuwa na siku iliyokuwa na majukumu chungu nzima tangu asubuhi saa kumi na mbili mpaka saa tatu na nusu usiku.

Mpaka nafika nyumbani ilikuwa ni saa nne na dakika zake. nimekuja kulala saa tano na dakika zake… ila nimestuka saa nane nikiwa na wazo ambalo sijataka kulipoteza, nikaamua niliandikie. tayari nimeshaliandikia na nimeshaliweka kwenye blogu ya SONGAMBELE.
https://www.songambele.co.tz/2023/11/nguvu-ya-vitu-vidogo-kuelekea-mafanikio-makubwa-katika-vitendo/

Baada ya kuwa nimeandikia hili wazo, nimeona nisirudi kulala. nikakumbuka wazo jingine nilolokuwa nalo jana wakati naendelea na shughuli, ambalo ndilo hili hapa, nikaamua kukaa chini kuliandikia pia, na hapa nipo bado naendelea kuliandikia. nikimaliza kuandika andiko hili, nitaliweka hewani hapa
https://wordpress.com/view/jifunzeuandishi.wordpress.com

Nitasoma kitabu kwa nusu saa mpaka saa moja, baada ya hapo sitakuwa na muda mwingine wa kuandika ambao ni rasmi kwa siku ya leo. Ratiba yangu ya leo inahusisha mikutano na watu wawili. mmoja nakutana naye asubuhi saa mbili, mwingine saa tano, na nitakuwa na majukumu mengine ….

Japo kwenye ratiba yangu sitakuwa na muda mwingine wa kuandika, ila nina uhakika sitakosa hata dakika kumi hapo katikati za kuandika hata makala fupi; Unajua kwa nini? Kwa sababu, inawezekana mmoja wa watu ambaye nimepanga kukutana naye akachelewa, ninaweza kuutumia muda huo kuandika kitu hata kama ni kidogo…

Inawezekana kwenye ratiba yangu, baadhi ya majukumu yakakamilika kabla ya muda wake uliopangwa, bado ninaweza kuutumia muda huo wa ziada kuandika, ila hata kama bado nitakuwa sijapata muda wa kuandika, kwa kuwa nimeshaandika hapa, siku ya leo hata ikipita, nina uhakika nimeweza kuandika kitu.

kitu kikubwa kwenye kuwa na muda wa kuandika ni kwamba unapaswa kutenga muda wa kuandika wewe mwenyewe. kwenye ratiba yako ya kila siku, weka muda wa kuandika. na muda huu siyo lazima uwe mwingi.

Watu wengi huwa wanafikiri kuwa wanahitaji muda mwingi kwa sababu hawana mwongozo sahihi wa kuwaongoza kwenye kuandika vitabu vyao. Ila kama utakuwa na mwongozo mzuri ambao unasaidia watu kwenye kuandika vitabu vyao, mwongozo kama kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. au kuwa kwenye jumuiya ya waandishi kama JIFUNZE UANDISHI, karibu kwenye jumuiya hii ya kipekee ya waandishi wanaondika. Unaweza kujiunga kwenye jumuiya hii ya kipekee hapa.
https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

4. Uandishi wa kitabu ni mgumu sana. Hiki ni kitu kingine ambacho huwa kinakuja kwenye akili za watu pale wanapokuwa wanafikiri kuandika kitabu, wanaanza kufikiri magumu yote ambayo yanahusiana na uandishi, basi wanaishia tu kutamani kama wangeweza kuandika kitabu ila hawaandiki. Ugumu huu unaanzia wapi? au watu wanaupata wapi…
Ugumu huu unaanzia chuoni.

Kama wewe umesoma chuo na ikafikia hatua ambapo ulipaswa kuandika desserttion yako ya chuoni. utakuwa unajua wazi kuwa haikuwa rahisi kuiandika.

Utakuwa uliipeleka kwa profesa na akaikataa mara kibao, inawezekana ilibidi urudie kuandika dessertaion yako mara nyingi na pengine ulichelewa kuhitimu tu kwa sababu hukuweza kuandika na kukamilisha kile ulichopaswa kuandika kwa wakati. Sasa hili umelibeba kwenye maisha yako ya kila siku, na unaambatana nalo kila sehemu unapoenda. Sikiliza, uandishi wa vitabu siyo mgumu kama ambavyo profesa wako amekuaminisha.

Ambatana nami profesa wako mpya kwenye uandishi wa vitabu ili uweze kuelewa nini hasa kinahitajika kwenye uandishi wa vitabu. Fanya yafuatayo ili uwe unajifunza kila siku kutoka kwangu kuhusiana na masuala mazima ya uandishi.

Kwanza; jiandikishe hapa ili usije kupitwa na makala zangu.

Pili, pata vitabu vyangu vya uandishi hapa. au wasiliana na 0678848396 au 0684408755 sasa ili upate nakala zako popote pale utakapokuwa.

tatu, jiunge na programu yetu ya uandishi ambapo ninaenda kukushika mkono kwenye uandishi wa kitabu chako mwanzo mpaka mwisho. unapaswa kuwa mmoja timu ya watu ambao ninawasimamia, jiunge kwenye programu hii hapa

au wasiliana na 0678848396

utaufurahia uandishi, uandishi ni raha bwana.

5. uchapaji wa vitabu ni ghaarama sana.
Wengi wanaosema hivi siyo waandishi. Ukweli ni kuwa uchapaji wa vitabu unahusisha mchakato kadha wa kadha, hata hivyo, ukweli ni kuwa gharama za uchapaji wa vitabu unaweza kuzipunuza kwa kuanza kuchapa kitabu chako kwa njia ya mtandao. niliwahi kuandika makala siku za nyuma nikieleza sababu kwa nini na wewe unahitaji kutoa kitabu chako kwa njia ya mtandao kwanza kabla ya kukitoa kwa njia ya kawaida.

Kama hukufuatilia hiyo makala, fanya hivyo sasa hivi hapa
https://youtu.be/43ouSGh5UAw?si=KLrO1dfwEFnPQjC5

Nadhani, kwa leo inatosha au wewe unasemaje? Una swali lolote ungependa kuuliza kuhusu uandishi? basi unaweza kuuliza hapa kwenye sehemu ya maoni au nitumie barua pepe jifunzeuandishi@gmail.com

karibu sana

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu programu yetu ya uandishi na kitabu kizuri cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MMBOBEVU basi, wasiliana nasi kwa 0678848396

karibu sana

Published by Godius Rweyongeza

Mimi Godius Rweyongeza, ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 15 kikiwemo kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Nimekuwa mwandishi kwa takribani miaka mitano sasa. Katika safari yangu ya uandishi nimeweza pia kusoma miswada ya watu mbalimbali na kugundua makosa mengi ya kiuandishi na hivyo nimeona pia ni muhimu kwangu kuanzisha blogu hii kwa ajili ya kuwasaidia waandishi wengi kujifunza uandishi na mbinu sahihi za kiuandishi. Blogu yangu kongwe iliyokuwepo kabla ya hii ni www.songambeleblog.blogspot.com Kama kweli uko makini na uandishi karibu ujiunge na kundi letu la waandishi makini. Tuwasiliane kwa 0755848391 Kama ungependa niusome muswada wako na kukupa mrejesho wa kitaalamu, tuwasiliane kupitia barua pepe ya songambele.smb@gmail.com au tumia namba ya 0755848391 Karibu

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started