Featured

Uandishi (Kuandika) raha

Rafiki yangu mpendwa, salaam, naamini unaendelea vizuri kabisa

Watu huwa wanapenda kutafuta na kupata raha kwenye maeneo mbalimbali. Wengine wanaenda mbali sana kwa kuhakikisha kwamba wanatumia vilevi kama pombe, sigara na madawa ya kulevywa.

Ila ukweli ni kuwa huhitaji kupata vilevi kama hivi ili uweze kupata raha. Kuna vitu vizuri ambavyo unaweza kufanya kama uandishi na ukapata raha idumuyo, raha isiyokuwa na dhambi hata kidogo.

Naamini wewe ni kama mimi ungependa kupata raha hii hapa. Basi kama ni hivyo, kuanzia leo hii anza kujifunza uandishi leo. Na kuna maeneo muhimu ambapo unaweza kujifunza uandishi kwa uhakika na kwa asilimia 100.

Kwanza na hapa kwenye hii blogu. Kila siku, ingia google, kisha andike JIFUNZEUANDISHI.WORDPRESS.COM ili uweze kufika hapa na kujifunza uandishi kwa undani wake. Kuna m akala nyingi ambazo unaweza kuanza kujifunza kwake hapa na kuchukua hatua.

Pili kama una swali au kitu chochote kile ambacho ungependa kuuliza kuhusu uandishi, basi unaweza kutuuliza. Tuandikie barua  pepe kwenda jifunzeuandishi@gmail.com, kisha uliza swali lako ulilonalo. Au unaweza kujaza fomu hii hapa chini na kuweka swali lako

Aidha tuna kundi maalum la telegram na linaitwa JIFUNZE UANDISHI, jiunge kwenye kundi hili kwa kubonyeza hapa

Lakini pia tuna kitabu kizuri kwa ajili yako ambacho kitakupa wewe mwongozo wa kujifunza uandishi kwa kina na kuweza kuufanyia kazi kwa uhakika. Kitabu hiki unaweza kukipata kwa kuwasiliana na 0684408755 sasa. Hiki kitabu ni mwongozo tosha wa ku kusaidia wew ekuanza kutimiza ndoto yako ya uandishi.

Aidha tuna pia kozi kwa watu maalumu wanaopenda kuandika kwa vitendo, hii ni kozi ambayo inatoa usimamizi kwa watu wanaopenda kuandika vitabu. Kwenye hii kozi tutakusimamia kwa ukaribu sana, kila siku utapokea masomo ya kipekee kutoka kwetu bila kuacha. Masomo mafupi ambayo unaweza kuyafanyia kazi. Kisha sisi tutakufuatilia kwenye uandishi wako kila siku kwa kukupa mrejesho wa kitalaam ambao utakusidia wewe kuweza kuboresha uandishi wako na kuufanya uzidi kuwa bora zaidi. Nafasi za kujiunga kwenye hii kozi siyo nyingi sana. Hivyo, tuwasiliane uone kama sasa hivi kuna nafasi kwa ajili yako.

Karibu sana

Kuandika raha

Uandishi raha

SOMA ZAIDI: KAMA UNAFIKIRI KILA KITU KILISHAANDIKWA, FIKIRI TENA (SABABU 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu na Tutaendelea Kuandika Vitabu, Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako)

Jinsi ya kupata kitu cha kuandika kila siku

Inawezekana wewe ni mfanyabiashara ambaye umekuwa unapeanda kuandika na kuweka maudhui kwa ajili ya biashara yako kwenye mtandao. Au pengine wewe ni mwandishi ambaye unaandika ila huwa unafikia hatua ambapo unatamani kuandika lakini hujui ni kitu gani uandike. Inawezekana unapenda uandike na kuitangaza biashara yako kwa watu wengi waweze kuifahamu, ila sasa unashindwa kufanya hivyo kwa sababu muda mwingine wewe hauna kitu cha kuandika.

Ni kwa namna gani unaweza kupata kitu cha kuandika kila siku kama mwandishi, mfanyabishara ambaye anatangaza biashara yake, au mtu tu ambaye ungependa watu wafahamu kuhusu wewe kipaji chako au chochote kile unachofanya.

Tuwe wakweli, bila kujali umekuwa na ujuzi kiasi gani kwenye ulimwengu wa uandishi. Huwa inafika hatua ambapo unajikuta kwamba unakosa kitu cha kuandika kabisa. Lakini ukweli ni kuwa kitu cha kuandika kinakosa kabisa pale ambapo unakuwa hauna mpangilio mzuri hasa linapokuja kwenye suala zima la uandishi. Kwenye makala ya leo, ninaenda kukuonesha jinsi ambavyo unaweza kupata kitu cha kuandika kila siku ili kuweza kuitangaza biashara yako na kuweza kuwafikia wengi zaidi.

Sehemu ya kwanza kabisa ya kupata kitu cha kuandika kila siku ni kupitia vitu ambavyo unasoma vitabuni. Kama wewe ni mwandishi au mfanyabiashara ni lazima kwa vyovyote vile unasoma vitabu na kujifunza kupitia vitabu kila siku. Sasa hili lichukulie kwa umakini mkubwa sana,

Kupitia vile unavyosoma kuna wazo ambalo unaweza kupata. Hili wazo, liandike pembeni ili ukifika muda wako wa kuandika uliandikie.

Lakini pia vile vitu ambavyo unaona kabisa vina nguvu kwako, viwekee alama kwenye kitabu unachosoma na baadaye unaweza kuvirudia kama sehemu yaw ewe kupata hamasa ya kupata kitu cha kuandikia kilasiku.

Kwa leo inatosha, kesho nitaendele na njia nyingine zinazokuonesha jinsi ya kuandika kila siku.

SOMA ZAIDI: Kuandika Ni Sanaa

Kwa nini unahitaji kuandika kitabu cha pili baada ya kuwa umeandika kitabu cha kwanza

Siri kubwa haipo kwenye kufanya jambo mara moja, bali kufanyajambo lilelile mara kwa mara. Floyd Mayweather ni mwanamasumbwi mkubwa sana hapa duniani. akiwa na rekodi ya kushinda 50-0. Na mara zote alikuwa anashinda kwa kishindo. Siri ya ukuu wake siyo kufanya mara moja bai ni kufanya jambo moja mara mara kwa marudio. Siri yake kubwa siyo ushindi wa mara moja, bali mwendelezo wa ushindi.

Hivyohivyo pia linapokuaja kwenye suala zima la kuandika kitabu. Huwa napenda kuwaambia watu kuwa haupaswi kuandika kitabu kimoja tu nakutulia, bali unapaswa kuwa na mwendelezo kwenye kuandika. Ndiyo maana huwa napenda kuwaambia watu kuwa baada ya kuwa umeweza kuandika kitabu chako cha kwanza, unapaswa kuandika na kitabu cha pili pia na hata kitabu cha tatu.

Kuna mtu anaweza asiwe makini unapoandika kitabu chako cha kwanza, lakini kitendo cha wewe kuandika na kutoa kitabu chako cha pili, kikamfanya achukue hatua na kutaka kukipata. Baada ya kusoma kitabu chako cha pili, mtu huyoihuyo akataka na vitabu vyako vingine vyote vya kwanza ambavyo umewahi kuandika.

Wengine ujumbe wako utawabariki kiasi kwamba kwenye maktaba zao watakuwa na vitabu vya kwako tu na baadhi ya waandishi wengine.

Kwa hiyo basi, usiache kuandika kitabu cha pili mara baada ya kuwa umeweza kuandika kitabu cha kwanza.

Huhitaji Kpmpyuta Ili Kuwa Mwandishi

Moja ya kitu ambacho watu huwa hawajui ni kuwa huwa natumia Zaidi simu kuandika kuliko ninavyotumia kompyuta. Sijui kwa nini lakini nadhani naweza kueleza kiufupi kwa nini niko hivi.

Mwaka 2016, wakati naanza kuandika sikuwa na kompyuta. Nilikuwa na simu kubwa ya kawaida ambayo ilikuwa inaisha chaji ndani ya saa moja la kuitumia. Hivyo, muda mwingi nilikuwa nalazimika kuitumia ikiwa kwenye chaji, ila simu hiii nilikuwa natumia kufanya mambo mengi sana, kusoma vitabu, kuandika Makala na vitabu, kuchapisha Makala mtandaoni na kuendesha mtandao wangu wa www.songambele.co.tz

Baadaye Nililkuja nikanunua simu nyingine nzuri Zaidi, nikawa naendelea kuitumia hii. Sikuwahi kumiliki kompyuta mpaka mwaka 2019 mwishoni. Rafiki yangu wa karibu pia alinunua kompyuta ambayo nilikuwa nikiazima, ila pale alipokuwa anaihitaji kwa ajili ya matumizi yake binafsi au kuangalia movie basi mimi nilikuwa siwezi kuitumia, kwa hiyo muda mwingi nilikuwa natumia simu kuandika kuliko kompyuta. Kwa kuwa nilikuwa natumia kompyuta za kuazima, nilijifunza kutumia kompyuta kwa ufanisi mkubwa, ili nikiwa Napata nafasi hata kidogo niweze kuandika kwa haraka, na kumaliza kazi zangu kwa wakati.

Lakini bado kuandika mara nyingi nilikuwa natumia simu yangu.  Leo hji karibia nina kila kifaa ambacho nakihitaji kwa ajili ya kuandika. Lakini bado najikuta nikitumia Zaidi simu kuandika kuliko ninavyotumia kompyuta. Muda mwingine naweza kuandika kwenye kompyuta na kuhariri kwenye sim una vitu vingine kama hivyo.

Nimeona niandike hili kwa ajili ya wale tu wanaosema kwamba hawawezi kuandika kwa sababu hawana kompyuta. Ukweli ni kuwa huhitaji kuwa na hivi vitu vyote. Simu yako ina uwezo mkubwa, itumie. Sikwambii hili ili kukuhamasisha tu, bali ni uhalisia ambao upo.

Leo hakikisha umepata kitabu cha ZAMA ZIMEBADILIKA; MAISHA YAMEBADILIKA; AJIRA HATARINI NA WEWE BADILIKA ili uweze kujifunza namna ya kudanndia teknolojia kwenye zama hizi. Pia leo hakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Kupata nakala yako, WASILIANA NA 0684408755

Fanya hivyo sasa.

Mimi natamani kuandika, lakini hata sijuia nianzie wapi?

Habari yako Rafiki yangu, na wewe wewe umekuwa ukitamani kuandika lakini hujuia wapi pa kuanzia, siku ya leo nina habari njema sana kwako Rafiki yangu.

Habari njema ni kuwa na wewe unaweza kuandika kwa kuanza na kile unachojua.

Ukwlei ni kuwa kuna vitu vingi ambavyo wewe unajua, na watu wengine watakuwa tayari kujifunza kutoka kwako.

Chukulia mfano wewe unajua mapishi mazuri ya chapati, ukweli ni kuwa unaweza kuwafundisha watu kitu hiki kwa kuwasaidia kuwaandikia kitabu.

Au tuchukulie mfano kuwa umekuwa unashona nguo kwa siku nyingi, hiki ni kitu ambacho unajua, unaweza kuwasaidia watu kushona nguo zao.

Unaweza bado ukawa unajiambia eti ndiyo kwanza umehitimu chuo, kwa hiyo unaandika nini. Andika hata kuhusu namna ulivyoweza kuishi Maisha yako ya chuo kwa miaka yote mitatu, minne au mitano uliyokuwa chuoni.

Ukweli ni kuwa huwezi kukosa cha kuandika. Kama bado unaona kwamba umefeli na unakosa kitu cha kuandika ila umekuwa ukitamani sna kuandika, basi usiwe na wasiwasi, tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili niweze kukusaidia kwenye hili.

Muhimu Zaidi, hakikisha umejipatia nakala ya kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Kina kila kitu unachohitaji kuhusu uandishi wa vitabu.

Nakala moja ni 20,000/- tu

Kupata nakala yako tuwasiliane kwa 0684408755 sasa

Ni gharama kiasi gani zinahitajika ili kuchapa kitabu chako ?

Anaandika mwandishi mbobevu GODIUS RWEYONGEZA
https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

Hili moja ya swali ambalo huwa napokea kila mara kutoka kwa waandishi na watu mbalimbali wenye ndoto za kuandika na kukamilisha vitabu vyao.

Ukweli ni kuwa hakuna gharama rasmi ambayo iko fixed ambayo naweza kukwambia hii ndiyo gharama rasmi ya uchapaji wa vitabu vyako. Ila kuna vitu vifutavyo ambavyo vitapekelekea gharama yako kuwa kubwa au ndogo.

Kitu cha kwanza ni UKUBWA WA KITABU CHAKO. Nadhani hili liko wazi na linajieleza. Kadiri kitabu chako kinavyokuwa kikubwa, ndivyo gharama yake ya uchapaji itakavyokuwa kubwa. Kitabu chenye kurasa 300, gharama yake ya uchapaji haiwezi kuwa sawa na kitabu chenye kurasa 100. Kumbe ukubwa wa kitabu ni mojawapo ya kipengele kitakachopelekea ghrama ya kitabu chako kuwa kubwa au ndogo.

KITU CHA PILI NI IDADI YA NAKALA UNAZOTOA. Kwa wachapaji wengi, kadiri unavyotoa idadi nyingi ya nakala ndivyo ambavyo ambavyo unakuwa na uwezekano wa kupunguziwa bei. Ukweli ni kuwa ukitoa nakala elfu moja, bei yake itakuwa chini kidogo ukilinganisha na ukitoa nakala mia moja.

KITU CHA TATU NI MCHAPAJI. Kila mchapaji ana bei zake. Hivyo, kulingana na aina ya mchapaji utakayemtumia pia, gharama yako itakuwa kubwa au ndogo.

KITU CHA NNE: ni aina ya kitabu unachotoa, je, ni kitabu ambacho unatoa na rangi kwa ndani au unatoa bila ya rangi. Kitabu cha rangi (coloured) bei yake inakuwa ni kubwa ukilinganisha na kitabu ambacho kinatolewa bila ya rangi.

Hivyo ndivyo vitu ambavyo hupelekea bei ya kitabu kuwa kubwa au ndogo.

NB: USHAURI WANGU: Kuna wachapaji wanakuruhusu kuchapa idadi ya vitabu kuanzia 50 au 100 na kuendelea….

Nashauri hasa kwa mwandishi anayeanza aitumie hii kama fursa. Zamani wachapaji walikuwa wanaringa.

Kama hutoi nakala elfu moja au elfu mbili au elfu tano hakubali kukutolea kitabu chako.

Siku hizi wapo wanaokuruhusu kutoa hiyo idadi ndogo. Kwako iwe fursa.

Unapotoa kitabu chako kwa mara ya kwanza usitoe nakala nyingi. Nakala 50 au 100 za kwanza zinatosha sana tu.

Zikiisha hizi utatoa nyingine. Nasema hili kutokana na aina ya soko la vitabu la Tanzania ambapo waandishi wengi huwa wanajikuta wanatumia gharama kubwa kuchapa vitabu ambavyo huwa vinawachukua miaka kutoka.

Juzi kuna mwandishi nilikuwa naongea naye akaniambia miaka miwili iliyopita alitoa nakala 2000 mpaka leo bado ana nakala 800.

Huhitaji uwekeze fedha zako nyingi sehemu moja hivi huku zikiwa zinarudi kidogo kidogo. Ndiyo maana nashauri uanze kutoa nakala kidogo kwanza, zikiisha utatoa nyingine. Huna cha kupoteza. Hata ukouza nakala 100 zote ndani ya wiki moja, unatoa hela unampa mchapaji anakutolea nakala nyingine ndani ya siku moja; kazi inaendelea.

Swali lako hapa litakuwa je, hivi vitabu vitakuwa na ubora.

Wengi naona wanajitahidi kwa ubora. Kutoa idadi nyingi za vitabu siyo ubora. Unaweza kutoa hela nyingi ili utolewe nakala nyingi na hado zikatoka zikiwa hazina ubora. Nina vitabu vya mtu mmoja ambaye alijikomba akatumia akiba yake kuchapa vitabu vyake kwa gharama kubwa ila vitabu vyake siyo bora.

Unachotakiwa kufanya ni kimpata mchapaji mzuri atakayechapa nakala zako chache kwa bei nzuri.

Kwa leo inatosha.

Maswali yote kuhusu uandishi wa vitabu yatumwe kwenye email ya jifunzeuandishi@gmail.com

Karibu sana
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz

Kuandika Ni Sana

Godius Rweyongeza
Anaandika mwandishi MBOBEVU
Godius Rweyongeza


https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

Rafiki yangu mpendwa salaam

Bila shaka unaendelea vizuri. Hongera sana kwa kazi nzuri unayoendelea nayo.

Siku ya leo ningependa tu kukwambia kuwa uandishi ni sanaa. Nimeona nikwambie hili kwa sababu moja ya changamoto kubwa ambayo huwa naiona kwa watu ni pale ambapo wanakuwa wanaandika vitabu vyao. Unakuta mtu anaanza vizuri, ila inapofika wakati wa kumaliza na kukamilisha kitabu chake anakwama.

Leo atakwambia naona kama kitabu changu bado hakijakamilika.
Mara atasema bado kuna kitu nataka niongezee kwenye kitabu changu.

Kesho kutwa atakwambia nahisi kitabu changu kinahitaji marekebisho mengi, na mengine mengi.

Ngoja nikwambie kitu kuhusu kazi za sanaa.

Hakuna kazi ya sanaa ambayo huwa imekamilika kwa asilimia 100. Ndiyo maana mimi nikisoma kitabu chako naweza kuona kama kuna kitu ambacho unaweza kuongezea, na msomaji mwingine pia akisoma kitabu chako ataona kama kuna kitu umeacha au unaweza kuondoa. Hiyo ni sanaa.

Wakati mimi kwa mfano naweza kuita kitabu change jina la UFUGAJI WA BATA NI HAZINA. Mwingine anaweza kuona kitabu hichohicho kiitwe UFUGAJI WA BATA NI UTAJIRI, mwingine akasema FUGA BATA KWA MANUFAA na mwingine akasema FUGA BATA UNUFAIKE Yote hiyo ni sanaa, hakuna ambaye tunaweza kumhukumu kwa kusema kuwa yuko sahihi au hayuko sahihi.

Na ndiyo maana huwa unakuta kwamba mwandishi mmoja ameandika kitabu, ila baadaye mwingine anaandika kitabu kingine ambacho nacho kina mambo mazuri kuhusiana na mada hiyohiyo ambayo mwandishi wa kwanza hakuyaandika.

Ndiyo maana kama mwandishi unapaswa kuwa msomaji mzuri wa vitabu.
Kuna kazi maarufu walizofanya watu maarufu kama akina Picasso. Nina uhakika kama Piccasso angekuwa anarudia kuchora kazi hizohizo leo hii, asingezichora kama zilivyo, bali angeziboresha…kwa sababu ni sanaa.

Mwandishi ambaye aliandika kitabu miaka 210 iliyopita, leo hii akikirudia anaona wazi kuwa angekuwa anaandika kitabu hicho hicho leo, basi angekiandika kivingine.

Kwa sababu uandishi ni sanaa kuna vitu ambavyo ningependa uepukane navyo. Vitu hivi ni kushindwa kutoa kazi yako kutokana na hali ya kuona kama vile haijakamilika inabidi ufikie hatua utoe kazi yako (kitabu chako). Na hili ili liwezekane unapaswa kujiwekea tarehe ya mwisho ya kukamilisha kazi yako.

Kwa mfano unapoanza kuandika kitabu chako unaweza kujipa mwaka mmoja tu kuandika kitabu.

Ukajiambia kuwa kufikia tarehe 1.11.2024 ninaenda kutoa kitabu changu, kadiri muda utakavyokuwa unakaribia ndivyo ambavyo utakuwa unajisukuma zaidi kuhakikisha umetoa kitabu chako, kama kuna vitu ulikuwa mwanzoni unazembea kufanya, utajikuta kwamba unajisukuma zaidi ili uweze kuvikamilisha.

Na siku ya kutoa kitabu chako ikifika itabidi ukitoe kwa maana kwa vyovyote vile hakuna kazi ya sanaa ambayo huwa imekamilika kwa asilimia 100. Siyo hata vitabu.

Ndiyo maana waandishi wa vitabu huwa wanakuna na toleo la pili, la tatu la nne, kuna vitabu vimeshakuwa na matoleo mpaka ya 20.

Ninachoweza kukwambia ni kimoja tu, andika kitabu chako, toa kitabu chako.

Kikubwa zingatia yale mambo yote ya msingi ambayo yanapaswa kuwa kwenye kitabu.
Unajua ni mambo gani haya?

Enewei njoo kwenye program yetu ya uandishi tukusaidia kuweza kufanikisha ndoto ya kuwa mwandishi mbobevu.

Anza kwa kujpatia nakala ya kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU kwa 20,000 tu. Wasiliana nasi kwa 0684408755

Kisha bonyeza hapa👇 kujiunga na program.
https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

Njia Bora Ya Kubobea Kwenye Uandishi

Ni shauku kubwa ya kila mmoja kuwa mbobezi kwenye uandishi. Ila ukweli ni kuwa huwezi kubobea kwenye uandishi bila ya kuandika. Kutaka kubobea kwenye uandishi bila kuandika ni sawa na kutaka kujenga misuli bila ya kufanya mazoezi. Ni kitu ambacho hakiwezekani!

Kitabu hiki cha JINSI  YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU ni mwongozo wa kuandika kwa watu wanaotaka kufanya vitu kwa vitendo. Kama wewe ni mtu wa kujifunza na kufanyia Kazi kile unachojifunza kwa vitendo, basi hiki kitabu kinaenda kuwa mwongozo mzuri kwako.

Ila kama wewe unajifunza bila ya kufanyia kazi, ni sawa utakisoma kitabu hiki, ila bila ya kukifanyia kazi, utakuwa umejinyima ile raha ambayo ungepata kwa kufanyia kazi moja kwa moja kile ambacho unajifunza.

Sasa nisikilize vizuri….

Nisikilize tena kwa umakini mkubwa sana.

Jipatie nakala ya kitabu hiki sasa hivi.

Gharama ya nakala hii ni 20,000/- tu. Tutakutumia nakala popote pale utakapokuwa hapa nchini, Tanzania na nje ya nchi.

Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Kujifunza Zaidi kuhusu uandishi, bonyeza hapa

Imani tano zisizo za kweli walizo nazo watu kuhusu uandishi vitabu…

Anaandika mwandishi Mbobevu
Godius Rweyongeza
0755848391
https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

Kuna imani tano kwenye ulimwengu wa uandishi ambazo zimezoeleka miongoni mwa watu ambazo si za kweli, ila zimeshika hatamu kama vile ni za kweli. Siku ya leo nipo hapa kuzieleza hizi imani kwa undani na mwisho wa siku kukupa suluhisho jipya kwa imani ambazo umekuwa nazo tokea mwanzo. Kiufupi ni kuwa nataka nizivunje hizi imani zako na nikupe imani mpya kuhusu uandishi wa vitabu, bila kuongeza la ziada, wacha tuzione…

1. Imani ya kwanza ni imani kuwa ili uandike kitabu unapaswa kuwa msomi. Siyo kweli kuwa ili uandike kitabu unapaswa kuwa msomi mwenye shahada kibao. Kuna wasomi wenye shahada nyingi kama hizo hawajaweza kuandika vitabu japo tulikuwa tunategemea kuwa waweze kuandika vitabu vya kutosha na vizuri.

Siyo jukumu langu kumhukumu mtu wala lakini msomi kama Robert Mugabe aliyekuwa na shahada saba tofauti alipaswa pengine kuwa ameandika vitabu vingi… Ila mpaka anaaga dunia hakuwa ameandika kitabu cchochote, ukweli ni kuwa kwenye kuandika kitabu chako unachohitaji siyo shahada. Unahitaji kuwa na ujumbe wowote ule unaoweza kuufikisha kwa watu…

Na wewe huwezi kukosa ujumbe wa kufikisha kwa watu, yaani kuwa ukose ujuzi wowote, ukose kuwa hata na kitu ambacho umekuwa unakifanya kwa siku nyingi…

Kama ukijisikiliza na kama ukijifiatilia vizuri, utakuwa na mengi. Naam mengi sana ya kuandika…

hata hivyo, ifahamike kuwa kama wewe ni msomi ujue pia wewe unategemewa sana kuandika na una mengi ya kuandika. Hivyo kwa ufupi ni kuwa msomi kwa asiye msomi anaweza kuandika kitabu. Unachohitaji ni maarifa sahihi ya namna ya kuandika kitabu chako. Unajiuliza ni kitu gani uandike?

Unaweza pengine ukawa hujui kitu gani uandike, ila mimi nina uhakika, nikikaa na wewe kwa dakika tano mpaka nusu saa, ninaweza kukupa mawazo lukuki ambayo ni ya kipekee kwako tu, ambayo hakuna mwingine mwenye nayo isipokuwa wewe tu. Upo tayari kunipa nafasi ya kukaa na wewe meza moja kwa dakika tano tu? Basi anza kwa kukaa nami kupitia hiki kitabu hapa, kama baada ya kusoma kitabu hiki utajiona huna kitu chochote cha kuandika. Ninaenda kukurudishia hela yako mara mbili. 100% guranteed!

2. Imani ya pili ni kuwa ili uandike kitabu unapaswa kuwa na umri umeenda….au umezeeka.

Sikumbuki ni mtu gani nilikuwa naongea naye siku za karibuni, ila akawa ananiambia kuwa ili kuandika kitabu chako unapaswa kuwa umestaafu na unakaribia kufa, tena nakwambia alinipa mpaka mifano, hahaha. Kuna kipindi watu walikuwa wanaamini ukiandika wosia unakuwa unakaribia kufa, kwa hiyo kijana kama mimi sipaswi kuandika wosia, ila nadhani hizi imani zimeisha jamani au huko kwenu vipi…..

Kuna watu wengi wanaamini kuwa ili uandike kitabu umri wako unapaswa kuwa umeenda. Uwe umestaafu na umefanya mambo katika ngazi ya kitaifa, kama mheshimiwa Mkapa, Mwinyi, Kikwete, na watu wengine wa aina hiyo….

Huwa wanasema hivi hasa wanapozungumzia kuandika historia ta maisha yako.

Ukweli ni kuwa huhitaji kuwa na miaka yote hiyo ili uandike historia ya maisha yako….
Kuna watu wameandika historia za maisha yao bila gata ya kuwa wanefikisha umri huo…

Unachohitaji siyo umri mwingi, bali nia kuamua kuandika kwani vitu vya kuandikia unavyo vingi. Unachohitaji wewe siyo uwe na historia kama ya Mkapa ili uandike historia yako.

Sikiliza, kama historia za watu wote zingekuwa kama za Mheshimiwa Mkapa au Mwinyi, sasa tunakuwa tunahitaji tuandike nini maana kila kitu si kinakuwa kinafahamika.

Lakini ukweli kuwa wewe huKwemda shule mpaka ilipotokea elimu ya watu wazima ndio unafanya historia ya maisha yako kuvutia watu.

Au ukweli kuwa kuna kipindi nyumbani mlikuwa hampati uji ndiyo utafanya historia yako kuwa pekee…

Huhitaji kuwa umesoma shule ya seminari kama Mkapa, ila ukweli kuwa ulisoma shule ya MTAKUJA na mwalimu alikuwa anakuja darasani amelewa na siku nyingine haingii darasani ndiyo unakupa historia ya kipekee.

Huhitaji kuwa ulipata shahada ya kwanza ukiwa na miaka 17, ila ukweli kuwa ulisoma chuo kikuu ukafeli na kufukuzwa ndiyo utafanya historia yako ya kipekee

Sikiliza, watu wengi wanatumua muda mwingi kutaka kuwa kama watu fulani badala ya kutumia muda mwingi kuwa wao wenyeewe. Kuwa wewe, andika kile ulichonacho na historia yako itakuwa ya tofauti. na huo ndiyo upekee ambao tutaukuta kwenye hisoria ya maisha yako..

3. Ninahitaji muda mwingi ili kuandika kitabu changu
Hii ni imani nyingine ambayo watu wanakuwa nayo. mtu anafikiri kwamba anahitaji muda mwingi ili kuandika kitabu chake na kukikamilisha, ukweli ni kuwa huhitaji kuwa na muda mwingi katika namna hiyo ili uweze kuandika kitabu chako. Ukweli mwingine zaidi ni kuwa hakuna mtu ambaye ana muda kama huo, mimi mwenyewe usije kudhani kuwa nina muda mwingi wa kutosha, mfano naandika andiko hili ukiwa ni usiku saa kumi kasoro dakika 18. Jana nililala saa tano baada ya kuwa na siku iliyokuwa na majukumu chungu nzima tangu asubuhi saa kumi na mbili mpaka saa tatu na nusu usiku.

Mpaka nafika nyumbani ilikuwa ni saa nne na dakika zake. nimekuja kulala saa tano na dakika zake… ila nimestuka saa nane nikiwa na wazo ambalo sijataka kulipoteza, nikaamua niliandikie. tayari nimeshaliandikia na nimeshaliweka kwenye blogu ya SONGAMBELE.
https://www.songambele.co.tz/2023/11/nguvu-ya-vitu-vidogo-kuelekea-mafanikio-makubwa-katika-vitendo/

Baada ya kuwa nimeandikia hili wazo, nimeona nisirudi kulala. nikakumbuka wazo jingine nilolokuwa nalo jana wakati naendelea na shughuli, ambalo ndilo hili hapa, nikaamua kukaa chini kuliandikia pia, na hapa nipo bado naendelea kuliandikia. nikimaliza kuandika andiko hili, nitaliweka hewani hapa
https://wordpress.com/view/jifunzeuandishi.wordpress.com

Nitasoma kitabu kwa nusu saa mpaka saa moja, baada ya hapo sitakuwa na muda mwingine wa kuandika ambao ni rasmi kwa siku ya leo. Ratiba yangu ya leo inahusisha mikutano na watu wawili. mmoja nakutana naye asubuhi saa mbili, mwingine saa tano, na nitakuwa na majukumu mengine ….

Japo kwenye ratiba yangu sitakuwa na muda mwingine wa kuandika, ila nina uhakika sitakosa hata dakika kumi hapo katikati za kuandika hata makala fupi; Unajua kwa nini? Kwa sababu, inawezekana mmoja wa watu ambaye nimepanga kukutana naye akachelewa, ninaweza kuutumia muda huo kuandika kitu hata kama ni kidogo…

Inawezekana kwenye ratiba yangu, baadhi ya majukumu yakakamilika kabla ya muda wake uliopangwa, bado ninaweza kuutumia muda huo wa ziada kuandika, ila hata kama bado nitakuwa sijapata muda wa kuandika, kwa kuwa nimeshaandika hapa, siku ya leo hata ikipita, nina uhakika nimeweza kuandika kitu.

kitu kikubwa kwenye kuwa na muda wa kuandika ni kwamba unapaswa kutenga muda wa kuandika wewe mwenyewe. kwenye ratiba yako ya kila siku, weka muda wa kuandika. na muda huu siyo lazima uwe mwingi.

Watu wengi huwa wanafikiri kuwa wanahitaji muda mwingi kwa sababu hawana mwongozo sahihi wa kuwaongoza kwenye kuandika vitabu vyao. Ila kama utakuwa na mwongozo mzuri ambao unasaidia watu kwenye kuandika vitabu vyao, mwongozo kama kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. au kuwa kwenye jumuiya ya waandishi kama JIFUNZE UANDISHI, karibu kwenye jumuiya hii ya kipekee ya waandishi wanaondika. Unaweza kujiunga kwenye jumuiya hii ya kipekee hapa.
https://chat.whatsapp.com/FkonMBpEW5i3kMztq8FkO3

4. Uandishi wa kitabu ni mgumu sana. Hiki ni kitu kingine ambacho huwa kinakuja kwenye akili za watu pale wanapokuwa wanafikiri kuandika kitabu, wanaanza kufikiri magumu yote ambayo yanahusiana na uandishi, basi wanaishia tu kutamani kama wangeweza kuandika kitabu ila hawaandiki. Ugumu huu unaanzia wapi? au watu wanaupata wapi…
Ugumu huu unaanzia chuoni.

Kama wewe umesoma chuo na ikafikia hatua ambapo ulipaswa kuandika desserttion yako ya chuoni. utakuwa unajua wazi kuwa haikuwa rahisi kuiandika.

Utakuwa uliipeleka kwa profesa na akaikataa mara kibao, inawezekana ilibidi urudie kuandika dessertaion yako mara nyingi na pengine ulichelewa kuhitimu tu kwa sababu hukuweza kuandika na kukamilisha kile ulichopaswa kuandika kwa wakati. Sasa hili umelibeba kwenye maisha yako ya kila siku, na unaambatana nalo kila sehemu unapoenda. Sikiliza, uandishi wa vitabu siyo mgumu kama ambavyo profesa wako amekuaminisha.

Ambatana nami profesa wako mpya kwenye uandishi wa vitabu ili uweze kuelewa nini hasa kinahitajika kwenye uandishi wa vitabu. Fanya yafuatayo ili uwe unajifunza kila siku kutoka kwangu kuhusiana na masuala mazima ya uandishi.

Kwanza; jiandikishe hapa ili usije kupitwa na makala zangu.

Pili, pata vitabu vyangu vya uandishi hapa. au wasiliana na 0678848396 au 0684408755 sasa ili upate nakala zako popote pale utakapokuwa.

tatu, jiunge na programu yetu ya uandishi ambapo ninaenda kukushika mkono kwenye uandishi wa kitabu chako mwanzo mpaka mwisho. unapaswa kuwa mmoja timu ya watu ambao ninawasimamia, jiunge kwenye programu hii hapa

au wasiliana na 0678848396

utaufurahia uandishi, uandishi ni raha bwana.

5. uchapaji wa vitabu ni ghaarama sana.
Wengi wanaosema hivi siyo waandishi. Ukweli ni kuwa uchapaji wa vitabu unahusisha mchakato kadha wa kadha, hata hivyo, ukweli ni kuwa gharama za uchapaji wa vitabu unaweza kuzipunuza kwa kuanza kuchapa kitabu chako kwa njia ya mtandao. niliwahi kuandika makala siku za nyuma nikieleza sababu kwa nini na wewe unahitaji kutoa kitabu chako kwa njia ya mtandao kwanza kabla ya kukitoa kwa njia ya kawaida.

Kama hukufuatilia hiyo makala, fanya hivyo sasa hivi hapa
https://youtu.be/43ouSGh5UAw?si=KLrO1dfwEFnPQjC5

Nadhani, kwa leo inatosha au wewe unasemaje? Una swali lolote ungependa kuuliza kuhusu uandishi? basi unaweza kuuliza hapa kwenye sehemu ya maoni au nitumie barua pepe jifunzeuandishi@gmail.com

karibu sana

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu programu yetu ya uandishi na kitabu kizuri cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MMBOBEVU basi, wasiliana nasi kwa 0678848396

karibu sana

Haya ni majuto ambayo unapaswa kuyaepuka

Sikiliza, watu huwa wanakuwa majuto mbalimbali hapa duniani, majuto ya vitu ambavyo hawakufanya, majuto ya hatua ambazo walikuwa wanaweza kabisa kuchukua ila hawakuchukua na mengine mengi.

Sitaki wewe uje uishi maisha ya majuto. Sitaki kabisaaa…

Ningependa unapoishi hapa duniani, uweze kutumia uwezo wako kwa viwango vikubwa… kuna majuto mengi ambayo nisingependa uje kuwa nayo, ila kwa leo kuna haya majuto ambayo nisingependa uwe nayo.

MAJUTO YA WEWE KUTOANDIKA KITABU.

Ngoja nikwambie kitu, hivi kwa mfano kama babu yako angekuwa ni mmoja wa watu ambao waliandika kitabu. Ungekuwa unajisikiaje kuhusu hilo? Ni wazi kuwa ungekuwa unajisikia vizuri sana. Mimi mwenyewe ningekuwa na kitabu ambacho aliandika babu yangu mngenikoma aisee. Hahaha

Yaani, ningekuwa naenda nacho kila sehemu, kila mtu angejua kuwa babu yangu aliandika kitabu na ningemuuzia hicho kitabu au kumpa zawadi. Nasema hili kutoka moyoni kabisa kwa sababu kwa stori ninazosikia kuhusu babu yangu, nina uhakika angekuwa ameandika kitabu, basi kingekuwa kitabu ambacho kinakonga nyoyo za watu wengi…

Ila hakuandika…

Mimi sijafanya hilo kosa na sitafanya hilo kosa.. nitaendea kuandika vitabu kila mara bila kuacha mpaka kieleweke….

KWA SABABU NAJUA NI HAZINA ambayo hata wajukuu wangu, watakuja kuikimbilia, na wataitumia kwa miaka mingi, KITABU NI HAZINA ISYOCHACHA.

Ubora ni kwamba kwenye ulimwengu wa leo tuna fursa nzuri za kuandika kitabu kuliko ilivyokuwa zama za babu zetu. NAJARIBU TU KUFIKIRIA kama babu yangu angeamua kaundika kitabu, angeanzaje, angeandika wapi kitabu chake, angekichapaje?

Hakuwa na vitu vizuri ambavyo tunavyo leo hii.

Kompyuta

Simu kubwa

Intaneti

Na vitu vingine kede kede tulivyonavyo…

Kumbe, kwenye uliwengu wa leo usipoandika kitabu, ni kosa lako. Kama unasoma huu ujumbe, ni wazi kuwa unausoma kwenye mtandao…

Na ni wazi kuwa una simu kubwa..

Hiyohiyo simu kubwa uliyonayo, unaweza kuitumia kwenye kuandika na kukamilisha kitabu chako.

Ndiyo maana nimeamua nikwambie leo kuwa usije siku moja kujuta kuwa nilikuwa naweza kuandika kitabu ila sikuandika.

Itumie hii fursa nzuri uliyonayo kuhakikisha kuwa unaandika, kitabu chako.

SOMA ZAIDI: Idadi Ya Kurasa Za Kitabu Unazopaswa Kuandika Mwaka Huu

Hkikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU, kupata nakala ya kitabu hiki na vingine vya uandishi tulivyonavyo wasiliana nasi kwa 0678848396

Kama ungependa kupata msaada wa kuandika kitabu chako au kutumia simu yako kwa usahihi kwenye kuandika kitabu chako. Basi usiwe na wasiwasi, tuwasiliane maana ni rahisi tu.0755848391. nicheki whatsap sasa au nipigie ili tumalize kila kitu

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye ni mwandishi mbobevu na ambaye anasaidia waandishi wengine kuweza kutimiza kusudi lao la kuandika vitabu vyao.

Unaweza kupata msaada wa kushikwa mkono na kuandika kitabu chako kama utakuwa mmoja wanafunzi kwenye CHUO CHA UANDISHI au kama utajiunga JIFUNZE UANDISHI. Kujiunga tuma ujumbe kwa namba ya simu 0755848391 au email jifunzeuandishi@gmail.com

Njia Sahihi Ya Wewe Kubobea Kwenye Uandishi

Rafiki yangu, unajiuliza ni kwa namna gani unaweza kubobea kwenye uandishi. Ni rahisi sana, njia bora na rahisi sana ya kubobea kwenye uandishi ni

Kwanza kuandika mara kwa mara. Usiandike tu mara moja na kuishia njiani, bali andika mara kwa mara bila kuchoka na bila kuishia njiani.

Pili kuonesha kazi zako unazoandika kwa watu. Kila unapokuwa unaandika kwa ajili ya kuonesha kazi zako kwa watu, utasukumwa kuandaa kazi zenye ubora ili watu wanapozisoma waweze kupata thamani kubwa kutoka kwenye hizo kazi. kwa hiyo, andika kazi, ila onesha pia hizo kazi zako kwa watu ili waweze kuziona. Huwi mwandishi kamili mpaka pale unapokuwa umeweza kuonesha kazi zako kwa watu wengine. Na waandishi wote unaowafahamu wewe, ni wale ambao walionesha kazi zao kwa watu.

Unaweza kufikiria kuwa kazi yako bado siyo bora na ya kipekee. Ukweli ni kuwa hata wale unaosoma vitabu vyao na kutamani vingekuwa vya kwako, leo hii wangekuwa wanarudia kuandika vitabu vyao, kuna marekebisho ambayo wao wanaona kabisa yanapaswa kuvanyiwa kazi. Nina uhakika mtu kama Shabaan Robert, angekuwa anarudia kuandika vitabu vyake leo hii, kuna mengi ambayo angeweza kurekebisha kulinganisha na mwanzoni.

Kwenye uandishi, kadiri unavyoandika ndivyo unazidi kuwa bora zaidi, hivyo ukirudia kusoma kazi zako za nyuma unaona wazi kuwa kuna marekebisho ambayo unaweza kuyafanya kwenye hizo kazi. Lakini huwezi kusema kuwa nasubiri niwe mkamilifu ili nije niandike. Ukweli ni kuwa hakuna kitu kama hicho. Andika, ili uweze kubobea.

Na tatu kujifunza mara kwa mara kuhusu uandishi. Hili ni jambo jingine na muhimu sana ambalo unatakiwa kulifanyia kazi bila ya kuacha. Unapaswa kujifunza mara kwa mara kuhusu uandishi. Kila mara, soma vitabu mbalimbalil vinavyozungumzia uandishi wa vitabu. Kadiri utakavyojifunza zaidi kuhusu uandishi, ndivyo utakavyozidi kubobea zaidi. Kuna usemi unaosema kuwa,  ukisoma vitabu 100 ndio unakuwa umeanza kulijua jambo, ukisoma vitabu 200 utaanza kujua kama unaweza kutengeneza fedha au la, ukisoma vitabu 300 unaanza kutengeneza kipato cha kawaida. Ukisoma vitabu 400 unatengenezda kipato cha uhakika na cha juu zaidi, na ukisoma vitabu 500 unakuwa mtu uliyebobea (world class). Je, wewe kwenye eneo la uandishi umesoma vitabu vingapi?

Rafiki yangu, hayo ndiyo mambo matatu ya uhakika yatakayokufanya uweze kuwa mwandishi mbobevu. Yafanyia kazi hayo kila siku bila yakuacha, kuna siku utakuja hapa na kunishukuru kw akile unachojifunza hapa.

Bila kuongeza la ziada, ningependa tu kukutakia siku njema sana.

Akhsante

kariu kwenye programu yetu maalumu ya kujifunza uandishi, ambapo utapata kushikwa mkono na mimi mwneyewe Godius Rweyongeza. kujiunga na programu hii ni rahisi sana, tuwasiliane kwa 0678848396

Karibu sana.

USHAURI MUHIMU: Kama una ndoto ya kuwa mwandishi na unawaza nani ATAHARIRI, ATACHAPA na jinsi utakavyouza kazi zako Basi Soma hapa.

Siku ya leo najibu swali nililoulizwa na mmoja wa wasomaji wangu. Anasema;

Hi Godius.
Naitwa Juma Mazengo Malale, kwa sasa nipo Shinyanga, ndoto yangu nikuwa mwandishi wa vitabu. Mpaka sasa nipo kwenye mchakato, changamoto ipo kwenye mambo kama haya.
1. Nani atahariri kazi yangu.
2. Nani atachapa.
3. Wapi nitauza.
4. Nitamudu gharama
5. Kitabu kibebe page ngapi?

 

Habari yangu ni njema ndugu yangu. Karibu kwenye ulimwengu wa waandishi na hongera sana kwa hatua hiyo uliyoamua ya kuwa mwandishi.

Hata hivyo pongezi zangu hupaswi kuzichukua zote kwa sababu kwa maelezo yako, inaonekana umeamua kuanza kuandika ila bado hujaanza kuandika; kitu ambacho ni muhimu sana,  linapokuja suala zima la uandishi.

Kiufupi hakuna mtu anaitwa mwandishi kwa sababu eti anatamani kuwa mwandishi au kwa sababu ana mpango wa kuja kuwa mwandishi siku moja. Kama ilivyo kweli kwamba hakuna mtu anaitwa mwanasheria kwa kutamani kuwa mwanasheria bali kwa sababu ameingia darasani, amesomea, amefuzu na anafanyia kazi fani yake.

Mwandishi ni mwandishi kwa sababu anaandika. Kwa hiyo, nataka na wewe uanze kuitwa mwandishi tena kuanzia leo, na utaweza hilo kwa kuanza kuandika.

Hatua hiyo moja tu itaweza kukufungulia fursa za kujua vitu vingine vingi. Kwenye swali lako umeuliza

1. Nani atahariri kazi yangu.
2. Nani atachapa.
3. Wapi nitauza.
4. Nitamudu gharama
5. Kitabu kibebe page ngapi?

Naweza kuanza kujibu maswali hayo baada ya kujihakikishia kuwa umeanza kuandika.

Kwa kuwa najua baada ya kusoma hapa utaendelea mbele na kuanza kuandika , basi acha niendelee kukujuza zaidi, ila sharti langu kwako ni moja tu. Uweke mpango wa kuandika mara tu baada ya kusoma makala haya.

UTAANDIKA KUHUSU NINI
Kuna maeneo mengi ambayo wewe unaweza kuandikia. Unaweza kuandika mengi kuhusu
👉maisha yako (maisha yako ni ya tofauti sana, unaweza kuwa unayachukulia poa, ila kuna mengi kutokana na maisha yako ambayo yanaweza kuwa msaada kwa watu wengine).

👉 Unaweza kuandika kuhusu ujuzi ulio nao ambao uliwahi kuupata kwa kufanya kazi fulani.

👉 Unaweza kuandikia eneo la taaluma yako. Kama kuna vitu umejifunza basi kuna watu wengine ambao wangependa kuvifahamu kwa kina hivyo vitu, unaweza kuwaelimisha watu kuhusu hivyo vitu kupitia maandishi yako.

👉 Unaweza kuandika kuhusu kitu unachopenda kufuatilia. Kama kuna kitu unapenda kufuatilia, basi unaweza kuamua kuzama ndani zaidi ili kukifuatilia hicho kitu huku ukiwa unawajuza wengine kwa kuwaandikia.

👉 Yapo mambo mengine ya kuandikia, ila kwa leo hayo yatoshe. Mengine utayasoma kwenye kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.

NANI ATAHARIRI KAZI YANGU
Wewe ndiye unapaswa kuwa mhariri wa kazi yako ukiwa mtu wa kwanza. Pia kuna wahariri watalaam ambao utawasiliana nao baada ya kukamilisha kazi yako, nao watakuwa tayari kukusaidia. Hivyo, Anza kuandika kwanza, ukifikia hatua ya uhariri wa kazi yako, itakuwa rahisi tu kukuunganisha na wahariri

NANI ATACHAPA KAZI YAKO
Wachapaji pia wapo wa kutosha. Anza kuandika kwanza na soma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 ili uweze  kupata zaidi mambo mengine kwa undani.

NITAMUDU GHARAMA
Ndio utaweza kumudu gharama.

KITABU KIBEBE PAGE NGAPI.
Itategemea unandikia nini na unataka kueleza mada kiundani kiasi gani. Binafsi nikiwa naandika kitabu huwa sifikirii sana kuhusu kurasa za kitabu. Ila huwa nafikiria zaidi kuhusu kile nilichonacho kuhusu mada husika. Huwa najitahidi kuandika kila kitu ninachojua na mwisho wa siku upande wa kurasa huwa unajipanga wenyewe. Ila kwa kuwa umeuliza kuhusu kurasa, basi acha nikwambie kwamba viwango vya kimataifa vya kuita kitu kitabu ni kurasa 50. Ila hili lisikuwazishe sana, Anza kuandika kwanza mambo mengine yanajipanga kadiri utakavyoendelea.

Kwa leo inatosha na ninakomea hapo. Hata hivyo, nakushauri sana, usome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Kitabu hiki kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na makala.

Kipate kitabu hiki kwa 6,500/- tu. Kupata kitabu hiki utatuma hicho kiasi kupitia 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Morogoro-Tz

0755848391

Somo Kubwa Kutoka Kwa 50 Cent Kwa Waandishi!!

Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene.

Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha.

Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki wanasisitiza ni kutoogopa.

50 Cent anasema kitu kikubwa ambacho unaweza kukiambatanisha na maisha yake ni kutoogopa. Yeye haogopi chochote kile maishani mwake. Na hicho kitu ndicho kimemfanya ashinde vikwazo ambavyo huwa hata vinawazuia watu kuchukua hatua ya kwanza.

Waandishi wanasisitiz kwamba, usiogope. Kamwe usiogope kabisaaa kwenye maisha yako.

Na mimi Leo napenda kukusisitiza kwamba usiogope

Kama wewe huwa unasoma Biblia, watalaamu wanakwambia kwamba kwenye Biblia Kuna USIOGOPE 365. Hivyo, hata Leo ulipoamka asubuhi, umeambiwa usiogope.

USIOGOPE

Kwa hiyo, kama wewe umekuwa unapanga kuandika kwa siku nyingi. Usiogope. Anza kuandika, andika, mwiso wa siku kila kitu kinawezekana.

KWA WAANDISHI WA VITABU:NI LUGHA GANI NZURI UNAPASWA KUTUMIA WAKATI WA KUANDIKA KITABU CHAKO?

Kuna watu huwa wanauliza ni lugha gani inafaa kutumia kwenye kuandika? Kiswahili au kiingereza?

Jibu la swali hili ni vigumu kulipata kwa mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuangalia
Watu uliowalenga.

Kama wasomaji wako wanajua vizuri Kiswahili Basi waandikie kwa Kiswahili, au la kama wanauelewa na kiingereza waandikie kwa kiingereza.

Kwa hiyo badala ya kujiuliza niandike kwa Kiswahili au kiingereza; jiulize wasomaji wangu ni watu wa aina gani? Je, wanaiweza lugha gani?

Tumia taarifa hizo kwenye kuandika kitabu chako.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 tuma elfu 5 kupata softcopy na elfu 15 kwa hardcopy.

Waandishi Wa Vitabu: Igeni Kitu Hiki Kimoja Tu Kutoka Kwa Wasanii Muziki

 

Huwa napenda kusikiliza muziki wa bongo flava mara mojamoja ninapokuwa nimepumzika. Kama na wewe huwa unausikiliza walau hata mara moja moja nyoosha mkono juu tujuane.

Ukifuatilia muziki huu hata kwa dakika tano tu, Kuna kitu kimoja ambacho utakigundua kwa wasanii na hiki ndicho ninataka tujadiliane leo. Kitu hiki siyo kingine bali ni kushirikisha kwa baadhi ya wasanii kwenye tungo zao mbalimbali.

Utakuta msanii fulani ameshirikiana na msanii mwingine kutoa tungo fulani. Ni kitu ambacho ukikiangalia kwa juu juu unaweza kuona ni cha kawaida au hakina maana, ila ukikiangalia kwa jicho la kipekee utagundua kuna kitu Kikubwa cha kujifunza hasa kwa WAANDISHI.

Labda tujiulize kwa Nini wasanii wa muziki huwa wanashirikiana? Sababu kubwa ni kupeana konekisheni na mashabiki.

Unakuta msanii A ama wafuasi na mashabiki wake huku msanii B akiwa na wafuasi na mashabiki wake pia. Sasa wanapoungana kutengeneza wimbo mmoja kuna wafuasi na mashabiki wa msanii A wataanza pia kumfuata na kumsabikia msanii B na hivyohivyo kwa upande wa pili.

Hakuna msanii anaogopa kushirikisha na mwenzake kwa kuogopa kuwa mwenzake ataondoka na wafuasi wake wote, badala yake wanashirikiana kadiri wawezavyo.

SASA WAANDISHI TUNAWEZA KUITUMIAJE HII?

Looo! Nimekumbuka kwamba naongea na waandishi na siyo wasanii wa muziki, ngoja sasa niache kuongelea masuala ya wasanii bwana niongelee mambo ya kiuandishi?

Kwa Waandishi mnaweza kutumia hii njia kwa kushirikisha katika kuandika makala.
Kuandika kitabu
Kuatangaziana bidhaa au vitu vyenu.
Kupost vitu vya mwenzako na mwenzako kupost vya kwako (hapa tafuta mwandishi ambaye mpo kwenye level moja au mnazidiana kidogo)
Kukomenti kwenye maandiko ya mwandishi mwenzako kwa kuongezea pointi za maana zaidi. Hii pia inaweza kukuongezea idadi ya watu wanaofuatilia kazi zako.
Kushiriki kikamilifu kwenye kundi la mwenzako na kutoa mafunzo.
Kuweka Dibaji kwenye kitabu chako; Dibaji iwe imeandika na mtu ambaye ana jina kubwa kuliko wewe.
Kuwaomba  Waandishi wengine wakuandikie neno fupi kuhusu kitabu chako (review).

Na mengine mengi.

Kwa hayo naamimi walau umelata kitu ambacho kinaweza kukusaidia Kama mwandishi.

Kama wewe MWANDISHI ambaye uko siriazi na kuandika na unataka kwenda viwango vingine, Basi hakikisha umesoma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.
Nakala laini (soft copy) inapatikana kwa 6500/- tu. Nakala ngumu kwa Sasa haipo. Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili upate nakala yako

KUZA KIPAJI CHAKO CHA UANDISHI

Kipaji ni mauwezo fulani hivi ya asili ambayo mtu unazaliwa nayo na yanakuwezesha kufanya vitu kwa namna ya upekee sana.

Mauwezo haya yanakutambulisha kwa watu kwa sababu hakuna mwingine ambaye anakuwa nayo. Na wala ya kwako hayawezi kulinganishwa na ya mtu mwingine.

Sasa nikuulize wewe, kipaji chako unakifahamu?

Ni kipi? Na je unakifanyia kazi?

Hakikisha unakitumia vizuri kipaji chako maana, siku ya mwisho utaulizwa namna ulivyokitumia kipaji chako😀😀.

Kujua namna nzuri ya kugundua na kutumia kipaji chako hakikisha umesoma kitabu cha KIPAJI NI DHAHABU Kimeeleza kwa kina jinsi ya Kugundua kipaji chako, kukinoa na kukitumia kwa manufaa.

Hardcocopy Ni 20,000/-

Softcopy ni 10,000/-

Rusha fedha sasa hivi kwa 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi

Siku kadhaa zilizopita nilipokea simu ya mtu aliyekuwa anataka nimwambie chuo kizuri kinachonoa Waandishi Wa Vitabu.

Nilimjibu vizuri tu, ila hakuridhika na majibu yangu kwa maana yalipingana na kile alichokuwa anaamini kwa asilimia 100. Yeye alitaka kwenda chuo, asomee uandishi na apate cheti. Cheti cha nini sasa? Najua, jamii yetu imezoea kwamba ukiwa na cheti basi hapo unakuwa umefaulu na unaenda ku-win maisha.

 Baada ya siku kama tatu hivi nilipokea ujumbe huu hapa chini kutoka kwa mtu mwingine.

Nadhani huyu alinifafuta na tuliongea kwa kina kuhusu hili.

. Simshauri kwa Sasa apoteze fedha zake kwenda chuo kwenda kusomea UANDISHI. 

Kuna kozi nyingi ambazo anaweza kusoma mtandaoni tena akiwa nyumbani, na akiwa anaendelea na shughuli zake za sasa. 

Ni sawa kuingia darasani, ila kwa sasa asifanye hivyo.

Afanye yafuatayo.

1. Aanze kuandika

2. Amtafute ‘mentor’ wa kumsaidia.

3. Aoneshe kazi zake anazoandika aidha mtandaoni au kwa watu wake wa karibu.

4. Apokee mrejesho wa kazi zake na aufanyie kazi.

5. Atumie mrejesho anaoupata na mafunzo anayopata kuboresha uandishi wake zaidi.

Kuna mengi ila kwa sasa hayo yanatosha.

Najua ushauri huu ataupuuza. Ila walau ninachofahamu kwa sasa atapoteza muda wake kwenda kujifunza uandishi kwa ajili tu ta kupata CHETI ambacho mwisho wa siku hakitamsaidia chochote.

Ngoja nieleze kitu zaidi hapa. Waandishi hawafahamiki Kama waandishi kwa sababu wanaVYETI. Waandishi ni waandishi kwa sababu wanaandika.

Mimi siyo mwandishi kwa sababu Nina cheti; HAPANA. Sijawahi hata siku moja kuona mtu ananiuliza cheti changu cha kuwa mwandishi kipo wapi😊😊. 

Kitu kingine ni kwa kuwa nguvu yake kubw ipo kwenye cheti kuliko kufahamu zaidi mchakato wa kuandika na kubobea kwenye uandishi, ataweka NGUVU kwenye kupata CHETI na atapata, ila hatakuwa mwandishi mzuri. Na hicho ndiyo kuantokea pia kwenye mfumo wa elimu. Wahitimu wengi wanahitimu na vyeti vizuri ila ujuzi SIFURI kutokana na ukweli kuwa waliweka nguvu kubwa kwenye VYETI kuliko kupata ujuzi.

🖊️🖊️🖊️🖊️🖊️🖊️

Nashauri asome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 ambacho kimeeleza kila kitu anachohitaji kujua kuhusu uandishi👇👇

Au awasiliane nami kwa 0755848391

Karibu kwenye darasa la mwisho la kuandika kitabu kwa mwaka 2021

Njoo ujifunze kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu

Kwa mara nyingine tena, napenda kukutangazia kuwa dirisha la kujiunga na darasa la uandishi limefunguliwa. Ila zamu hii litakuwa darasa la mwisho kwa mwaka 2021.

Kama una mpango wa kuandika kitabu kabla mwaka haujaisha, Basi jiunge na darasa hili.

Nani anahitajika kwenye darasa?

Mtu yeyote mwenye nia ya kuandika kitabu na kujifunza mambo yote yanayoendana na uandishi.

Darasa litaanza lini na litafanyikia wapi?
Darasa letu huwa linafanyikia WhatsApp na sasa hivi tumeongeza kipengele cha kujifunza kupitia telegram pia.

Kwa darasa hili ambalo ni la mwisho kwa mwaka huu, tunategemea litaanza kati ya tarehe 15-20 mwezi 10. Wanadarasa tukishatimia tutapanga tarehe rasmi ya kuanza kati ya hizo, ila itakuwa kati ya 15-20 oktoba.

Wanahitajika watu wangapi darasani?
Wanahitajika watu watano tu. Darasa likijaa limejaa, kutakuwa hakuna nafasi ya ziada.

Kuna gharama yoyote ya kuhudhuria darasa hili?
Ndiyo. Kwa kawaida darasa hili huwa linalipiwa elfu sabini (70,000). Ila zamu hii wahudhuriaji wote wanapewa ofa ya kuhudhuria darasa hili kwa elfu hamsini tu (50,000/-)

Mfumo tunaoutumia ni wa first come, first served

Karibu ujihakikishie nafasi kwa kulipia kupitia 0755848391.

Kinachokukwamisha wewe kuandika kitabu chako ni hiki

Kama kuna kitu ambacho kinakukwamisha wewe kuandika kitabu chako siyo kitu kingine bali ni hiki. Hujakaa chini na kuamua kuandika kitabu chako.

Ngoja nikwambie kitu, haijalishi una wazo zuri kiasi gani la kitabu, unapaswa kukaa chini na kuliandikia. Wazo kama wazo halitajiandikia.

Sasa kitu ambacho unapaswa kufanya sasa, Ni kukaa chini na kuliandika wazo lako.

1. Anza kuandika

2. Usihukumu mawazo yako wakati wa kuandika mpaka pale utajapomaliza.

3. Usihariri mpaka umalize kuandika

4. Andika mpaka pale unapohisi umemaliza kila kitu.

5. Usihariri wakati wa kuandika

6 Anza kuandika leo.

Kwa Nini Nitaendelea Kuandika Kila Siku Bila Kuchoka

Leo nimeona nishirikishe kuhusu uandishi na kwa nini nitaendelea kuandika bila kuchoka.

1  Uandishi Ni kitu ambacho ninafanya kutoka moyoni

2. Uandishi ni kitu ambacho kinanipa ushindi. Hata kama ikitokea jdani ya siku yangu nimeshindwa kufanikisha majukumu yangu ila nitakuwa na uhakika kuwa kwenye suala zima la uandishi nimefanikiwa kwa kuandika kitu fulani.

3. Uandishi unanifanya nifikirie nje ya boksi.

4. Uandishi unanifanya nione cha kuandika kwenye yale ambayo wengine  wanaona hayafai.

5. Maandiko yangu ni msaada mkubwa kwa watu wengine

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri

Design a site like this with WordPress.com
Get started